Rais Samia atengua uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri 4 nchini

0
174

Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Wakurugenzi 4 wa Halmashauri kwa matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo hususan za ustawi na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Wakurugenzi hao ni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Mkoani Mwanza, Manispaa ya Singida – Mkoani Singida, Halmashauri ya Jiji la Mbeya – Mkoani Mbeya na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa.

Akizungumza mbele ya Rais, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Innocent Bashungwa amesema halmashauri zote ambazo zimetuhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha za miradi uchunguzi umefanyika na kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita uchunguzi unaendelea.

Rais Samia ameagiza uchunguzi uendelee katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo pia kuna tuhuma za namna hiyo.