Rais Samia atatua changamoto ya afya Itiso

0
222

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chamwino mkoani Dodoma, Deo Ndejembi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumaliza changamoto ya kituo cha afya katika kata ya Itiso iliyopo katika jimbo hilo.

Amesema baada ya kusikia changamoto ya kituo cha afya iliyokua inawakabili Wananchi hao wa Itiso, Rais Samia Suluhu Hassan alielekeza shilingi milioni 250 zipelekwe kwenye kata hiyo kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.

Naibu Waziri Ndejembi ametoa shukrani hizo kwa Rais Samia Suluhu Hassam wakati akizungumza na wakazi wa kata za Ikombo na Itiso, ambapo pia aliwaeleza mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya sita madarakani.

“Hapa Itiso hapakuwahi kuwa na kituo cha afya, iliwalazimu msafiri umbali mrefu kwenda kata nyingine ya Haneti, Mimi niliwaahidi wakati wa kampeni kuwa tutajenga kituo cha afya, leo namshukuru Rais Samia nilipobisha hodi akasema akakubali kutupatia shilingi milioni 250 kutoka kwenye makato ya tozo kwa ajili ya ujenzi huu.” amesena Naibu Waziri Ndejembi