Rais Samia ataka uwazi katika mikataba ya TARURA

0
171

Samia Suluhu Hassan amewataka watendaji wa TARURA kuhakikisha mikataba yote 960 iliyotangazwa huku kumi ikisainiwa leo mbele yake inakuwa ya uwazi na orodha ya makandarasi waliopatikana inatangazwa kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wake.

Aidha Rais Samia ameitaka TARURA kutoa orodha ya makandarasi waliowahi kuharibu ujenzi wa miundombinu ili wasipewe tena kazi sambamba na kuonya tabia ya kuwepo kwa madalali wanaotoa zabuni kwa watu wasio na uwezo wala sifa.

Pia amemweleza Mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff kujihakikishia nafasi aliyonayo kwa kusimamia vema miradi hiyo sambamba na kuwataka wakandarasi wazawa kubadilika na kujenga barabara za kudumu na zenye kutumia teknolojia japo kwa miaka 10 badala ya mazoea ya ujenzi wa barabara za msimu zinazoisababishia serikali gharama za mara kwa mara.