Rais Samia: Askari wenye vitambi warudi hapa kuviondoa

0
138

Rais Samia Suluhu Hassan, amemuagiza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala, kuhakikisha askari wote waliopo kwenye jeshi la uhamiaji ambao wana vitambi warudi chuoni hapo kufanya mazoezi ili kuviondoa na kuwa wakakamavu.

Rais Samia ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya awali ya askari wa Uhamiaji kozi namba 01/2021/2022.

Pia amesema askari wajengewe utaratibu wa kurudi vyuoni kwenye kozi fupi za mara kwa mara, ili kuwa tayari wakati wowote.