Rais Samia apewa tuzo ya heshima na NDC

0
211

Rais Samia Suluhu Hassan amepewa tuzo ya heshima na Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kwa kutambua na kuthamini mchango wake wa kuendeleza chuo hicho.

Wengine waliopewa tuzo hiyo ni pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete, Rais wa awamu ya Tano Hayati Dkt. John Magufuli, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein, Wakuu wa Majeshi wastaafu, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Ombeni Sefue na wakuu wastaafu wa chuo cha Taifa cha Ulinzi.

Wengine waliotambuliwa kwa mchango wao katika chuo hicho ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha na Makamu Mkuu Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala.