Rais Samia amewaapisha aliowateua

0
167

Rais Samia Suluhu Hassan, leo amewaapisha wakuu wa mikoa pamoja na Makatibu Tawala wa mikoa wapya aliowateua hivi karibuni.

Hafla ya kuwaapisha viongozi hao zimefanyika Ikulu mkoani Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Wakuu wa mikoa walioapishwa hii leo ni Nurdin Babu anayekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Fatma Mwasa anayekuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro, Halima Dendego anayekuwa mkuu wa mkoa wa Iringa na Meja Jenerali Suleiman Mzee anayekuwa mkuu wa mkoa wa wa Mara.

Wakuu wa mikoa wengine walioapishwa ni Peter Serukamba mkuu wa mkoa wa Singida, Kanali Ahmed Abbas Ahmed mkuu wa mkoa wa Mtwara,
Kanali Laban Thomas mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Albert Chalamila mkuu wa mkoa wa Kagera na Dkt. Yahaya Nawanda ambaye ameapishwa kuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu.

Viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mauungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma.

Jalai 28 mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan alifanya uteuzi wa wakuu wa miikoa wapya tisa , kuwahamisha vituo vya kazi wakuu wa mikoa saba na wengine 10 aliwabakiza kwenye vituo vyao vya kazi.

Pia aliteua Makatibu Tawala wa mikoa wapya saba na kuwahamisha vituo vya kazi Makatibu Tawala wa mikoa 10 na wengine tisa kubakia kwenye vituo vyao vya kazi.