Rais Samia aipongeza hospitali ya Rufaa Manyara

0
126

Rais Samia Suluhu Hassan amewapongeza watumishi wote wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Manyara (Manyara RRH) kwa kutoa huduma bora na kuwataka waendelee kuwa na moyo wa kujitolea wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Akiwa hospitalini hapo, Rais Samia ametembelea wodi ya watoto kwa lengo la kuwajulia hali ambapo pia ametaka kufahamu ubora wa huduma wanazozipata.

Akitoa taarifa ya hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa wa Manyara, Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Catherine Magali amesema kuwa, upatikanaji wa dawa hospitalini hapo ni asilimia 97.

Ujenzi wa majengo mengine ya hospitali hiyo bado unaendelea, na unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 10.5 hadi kukamilika kwake.

Tayari serikali imeshatoa shilingi bilioni 5.5 kwa ajili ya ujenzi huo.

Rais Samia Suluhu Hassan anakamilisha ziara yake ya siku mbili mkoani Manyara hii leo na ataelekea mkoani Arusha.