Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi mbalimbali

0
403

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali ambapo amemteua Prof. Ahmed Mohamed Ame kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA). Prof. Ame ambaye ni Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
anachukua nafasi ya Mhandisi John Nduguru.

Amemteua pia Eliud Sanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Airtel Tanzania, akichukua nafasi ya Gabriel Malata aliyeteuliwa kuwa Jaji.

Sanga ni Mkurugenzi wa zamani wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSF).

Aidha, Rais amemteua Jaji (Mstaafu) Mathew Pauwa Mhina Mwaimu kuwa Mwenyekiti na Mohamed Khamis Hamadi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kipindi cha pili.

Wakati huo huo, Rais amewateua Thomas Paulo Masanja, Amina Talib Ali, Khatibu Mwinyi Khatibu na Nyanda Josiah Shuli kuwa Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu ameeleza kuwa uteuzi huu ni kuanzia Januari 15, 2023.