Rais Samia afanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu UN

0
195

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Amina Mohammed, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Katika mazungumzo hayo Amina amewasilisha salamu kutoka kwa Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres na kumponeza Rais Samia kwa kushika nafasi ya urais na kumtakia heri katika majukumu yake.

Amina amemhakikishia Rais Samia kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono katika jitihada zake mbalimbali ikiwemo kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).