Rais Samia atembelea bunge la Msumbiji

0
649

Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anaendelea na ziara yake ya kiserikali ya siku tatu nchini Msumbiji, leo ametembelea Bunge la nchi hiyo na kupata fursa ya kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa bungeni hapo.

Akizungumza na Rais wa Bunge la Msumbiji Esperanca Laurinda Francisco Nhiuane Bias, Rais Samia amesisitiza ushirikiano baina ya bunge hilo na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema ni muhimu kwa mabunge hayo kufanya kazi kwa pamoja, hatua itakayosaidia kupatikana kwa maendeleo ya pande zote mbili.

Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza mabunge ya Tanzania na Msumbiji kukutana, ili kufanyia kazi masuala mbalimbali ambayo amezungumza na Rais wa bunge hilo la Msumbiji.