Rais Samia Suluhu Hassan amemtaka Waziri wa Fedha, Dkt Mwigulu Nchemba kutanua wigo wa ukusanyaji wa kodi na kuhakikisha hakuna nguvu kubwa inayotumika katika kudai kodi kutoka kwa Wafanyabiashara.
Ameonya tabia ya baadhi ya Watendaji wa Serikali kufunga biashara, kuchukua fedha za Wafanyabiashara, kuchukua vifaa vyao vya kazi na kufunga akaunti zao, jambo linalosababisha Wafanyabiashara wengi kuhamia nchi jirani.
Amesema anachotaka ni kuona idadi ya Wafanyabiasha inaongezeka na Wafanyabiashara hao wanafanya shughuli zao katika mazingira rafiki.
Rais Samia ametoa agizo hilo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma baada ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi, Mawaziri na Naibu Mawaziri aliowateua hapo jana.