Rais Samia aanza ziara ya siku 3 Kagera

0
140

Rais Samia Suluhu Hassan amewasili Mkoani Kagera tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu.

Rais Samia amepokelewa na wananchi pamoja na viongozi wa mkoa wa Kagera na Kisha kupata fursa ya kuzungumza nao.

Akisalimiana na Wananchi wa wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera, Rais Samia amesema serikali itahakikisha inawaletea wananchi maendeleo na hasa huduma za kijamii.

Rais Samia akiwa Mkoani Kagera atakagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuongea na wananchi katika maeneo tofauti Mkoani humo.