Rais Samia aanza ziara Kigoma

0
149

Rais Samia Suluhu Hassan ameanza ziara yake mkoani Kigoma, ambapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa kufungua hospitali ya wilaya ya Kakonko iliyopo katika kijiji cha Itumbiko ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake.

Pia atafungua mradi wa maji katika eneo la Kanyamfisi – (Kakonko Mjini).

Kazi nyingine atakayoifanya ni kufungua barabara ya Kabingo – Nyakanazi na kuzungumza na wananchi.

Ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya Kibondo (Mjini) – Nduta yenye urefu wa kilomita 25.9 na atahitimisha siku yake kwa kuzungumza na wananchi katika
uwanja wa Taifa Kibondo.