Rais RAMAPHOSA wa AFRIKA KUSINI kuwasili nchini Tanzania Agosti 14 kwa ziara ya kikazi ya siku 2

0
284

Rais CYRIL RAMAPHOSA wa AFRIKA KUSINI anatarajia kuwasili nchini keshokutwa Jumatano ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku mbili kabla ya kuhudhuria kikao cha wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kusini mwa Afrika -SADC.

Mkuu wa mkoa wa DSM, PAUL MAKONDA amesema atakapowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Rais RAMAPHOSA atalakiwa na mwenyeji wake Rais Dkt. JOHN MAGUFULI.