Rais Ramaphosa naye amzungumzia Dkt Magufuli

0
190

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema alifurahishwa na tabia ya Dkt John Magufuli ya kutopenda kusafiri kwenda nje ya nchi, badala yake alipenda kubaki hapa nchini ili kujenga Taifa lake.

Amesema ameona kwa macho matokeo ya tabia ya Dkt Magufuli ya kupenda kubaki Tanzania akichapa kazi, hali ambayo imelipatia Taifa lake maendeleo makubwa.

Rais Ramaphosa amesema Watanzania wanapaswa kuwa na furaha kubwa kuliko watu wote, kwa kupata Kiongozi aliokuwa akiwapenda na kuwatumikia katika muda wote wa maisha yake.

Kwa mujibu wa Rais Ramaphosa, Dkt Magufuli alisimama kama shujaa wa Afrika katika vita dhidi ya rushwa na ubadhilifu wa mali ya umma.

Amesema pia katika uongozi wake Dkt Magufuli alionyesha njia kuwa viongozi wanapaswa kuwatumikia Wananchi na sio kujitumikia wenyewe.