Rais Nyusi aanza ziara nchini

0
192

Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji, amewasili nchini hii leo kuanza ziara yake ya siku mbili.

Katika uwanja wa ndege wa Geita, Rais Nyusi amepokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, akiwa hapa nchini Rais Nyusi atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Dkt Magufuli.

Katika uwanja huo wa ndege wa Geita, Rais Nyusi amepata fursa ya kushuhudia burudani iliyotolewa na vikundi mbalimbali.