Rais Mwinyi akoshwa na wafanyabiashara wadogo

0
177

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema amefarijika kuona wafanyabiashara wadogo wakiboresha biashara zao kuanzia uzalishaji wa bidhaa hadi vifungashio vya bidhaa hizo kwa ajili ya kuzipeleka sokoni, akitaja chanzo cha mabadiliko hayo kuwa ni jitihada zinazofanywa na taasisi husika zinazosimamia biashara hizo.

Ameyasema hayo alipotembelea mabanda ya wafanyabiashara katika viwanja vya maonesho ya 46 ya biashara Kimataifa maarufu sabasaba yanayoendelea mkoani Dar es Salaam.

Rais Mwinyi ameongeza kwa kusema kuwa Serikali inayo utayari wa kuendelea kuboresha mazingira ya wawekezaji nchini kwa kuweka mazingira rafiki ikiwemo kupunguza muda wa kupata vibali, kuwapatia wawekezaji maeneo ya ardhi kwa wakati na hivi sasa maeneo mengi yamekwisha tengwa kwa ajili ya viwanda.

Leo ni siku ya saba ya maonesho ya Sabasaba yanayoendela mkoani Dar es Salaam.