Rais Museveni wa Uganda kuwasili nchini kesho

0
412

Rais Yoweri Museveni wa Uganda, kesho Julai 13 anatarajiwa kuwasili hapa nchini kwa ziara binafsi ya siku moja.

Katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita, Rais Museveni atapokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt. John Magufuli na baadae kuwa na mazungumzo binafsi na mgeni wake.