Rais mstaafu Benjamin Mkapa Kuzikwa kijijini kwao Lupaso

0
202

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa amesema kuwa mwili wa rais mstaafu Benjamin William Mkapa utazikwa siku ya jumatano Julai 29,2020 kijini kwao Lupaso wilayani Masasi mkoani Mtwara.

Majaliwa amesema mwili wa Mzee Mkapa utaagwa siku tatu kuanzia tarehe 26 hadi 28 katika uwanja wa uhuru,wananchi watapata fursa kwa siku zote hizo tatu.

Ratiba iliyotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, inaonyesha kwamba shughuli ya kuaga mwili wa rais mstaafu Mkapa itafanyika katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam ambako wananchi mbalimbali watapata fursa ya kujitokeza na kumuaga kiongozi wao huyo mpendwa.

Rais Mkapa enzi ya utawala wake, alisifika kwa kauli mbiu ya ukweli na uwazi. atazikwa Jumatano mchana katika kijiji alikoanzia maisha kijiji cha Lupaso wilaya ya Masasi.

Wakati huu ambapo Taifa likiwa kwenye maombolezo ya siku saba, salamu za rambirambi zinaendelea kutolewa nchini kutoka sehemu mbalimbali, huku baadhi ya viongozi waliowahi kufanya kazi chini ya utawala wake wakikumbusha namna rais huyo alivyolikwamua taifa kiuchumi.

Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete ambaye wakati wa utawala wa Rais Mkapa alikuwa waziri wa mambo ya nje, amesema taifa limeondokewa na kiongozi wa aina yake na amewasihi watanzania kuendelea kuyaenzi yale yote aliyoyaasisi