Rais Magufuli ateuwa viongozi watatu

0
263

Rais Dkt. John Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi watu kusimamia na kuongoza mabaraza ya Vyuo vikuu vitatu hapa nchini.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Rais Magufuli amemteua Rais wa Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein Kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kuchukua nafasi ya Jaji Mstaafu Barnabas Samatta ambaye amemaliza muda wake.

Rais Magufuli pia amemteua Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikkuu cha Afya na Sayansi Shirikishi-MUHAS kuchukua nafasi ya Mariam Joy Mwafisi ambaye amemaliza muda wake

Mwisho Rais Dkt. John Magufuli amemteua Bi Gaudensia Kabaka kuwa mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma-UDOM kwa kipindi cha pili.