Rais Magufuli: nimewasamehe Makamba na Ngeleja

0
169

Rais John Magufuli amesema kuwa amewasamehe Wabunge January Makamba wa Bumbuli mkoani Tanga na William Ngeleja wa Sengerema mkoani Mwanza, kwa kile alichoeleza walimtukana kwenye simu.

Rais Magufuli ameyasema hayo jijini Dar es salaam, wakati akifungua mkutano wa mashauriano baina ya Bodi ya Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Bodi ya Makandarasi (CRB) na Bodi ya Wahandisi (ERB).

“Nakumbuka hivi karibuni kuna watu walinitukana na nikapata uhakika kwamba sauti zile ni zao, nikafikiria nikasema hawa wakipelekwa kwenye kamati ya siasa adhabu itakuwa kubwa, walinitukana kwenye simu na nikahakikisha ni kweli ni sauti zao lakini nimewasamehe”, amesema Rais Magufuli.

“Lakini wakajitokeza wawili wakaniomba msamaha, nikasema nisipowasamehe nitabaki na maumivu makubwa sana, watu hao ni January Makamba na William Ngeleja nikaona niwasamehe tu, waliomba msamaha nikasema ni vijana nimewasamehe” ameongeza Rais Magufuli.

Amesema kuwa, kama kulikua na mambo mabaya kipindi cha nyuma ni vema kuyasahahu ili kuanza upya maana kusamehe siyo jambo rahisi lakini saa nyingine inabidi usamehe.