Rais Magufuli mgeni rasmi kwenye mashindano ya kusoma Quran

0
291

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amejumuika na waislamu katika uwanja wa Taifa Dar es salaam kushuhudia mashindano ya 20 ya kusoma Quran, huku mshindi wa kwanza wa mashindano hayo akitarajia kunyakuwa shilingi milioni 20

Maelfu ya Watanzania wamejitokeza uwanjani hapo kushuhudia tukio hilo linaloendelea hivi sasa, viongozi mbalimbali wameungana na Rais Magufuli katika mashindano hayo, akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais wa awamu ya tatu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete sambamba na Mufti wa Tanzania Alhaj Sheikh Abubakari Zuberi bin Ali .