Rais Dkt. JOHN MAGUFULI ametoa wito kwa viongozi wote wa awamu ya tano kufanya kazi kwa karibu na wawekezaji pamoja na wafanyabiashara nchini bila kuwawekea urasimu usio na sababu.
Akizindua kiwanda cha kusaga nafaka cha 21st Century FOOD AND PACKAGING kilichopo KURASINI jijini DSM, Rais MAGUFULI amewataka wawekezaji kuja zaidi kwani serikali ya awamu ya tano ipo tayari kufanya nao kazi.
Uzinduzi wa kiwanda hicho umeenda sambamba na Jubilee ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Kampuni ya METL ambapo Mgeni Rasmi Rais John Magufuli ametoa wito kwa kampuni za METL kulima ngano hapa nchini badala ya kuendelea na utaratibu wa sasa wa kuagiza Ngano kutoka nje ya nchi.
Awali Mkurugenzi wa kampuni za METL, MOHAMED DEWJI amesema jumuiya ya wawekezaji nchini wanafurahishwa na kasi ya ujenzi wa miundombinu inayoendelea hapa nchini hasa katika kipindi hiki cha awamu ya Tano
Kampuni za METL zimeajiri wafanyakazi zaidi ya elfu thelathini mpaka sasa na ilianza kusaga tani 240 za Nafaka mwaka 2005.