Rais Dkt. John Magufuli amesema kukamilika kwa mradi wakufua umeme wa mto Rufiji kutashusha bei ya umeme na kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda nchini.
Akizungumza wakati wa uwekaji jiwe la msingi la mradi wakufua umeme wa maji katika mto Rufiji mpakani mwa mikoa ya Pwani na Morogoro, Rais Dkt. Magufuli amesema uhaba wa umeme unasababisha kupanda kwa bei ya bidha viwandani.
Mradi huo wenye megawati 2,115 unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi trilioni 6.5 ni moja ya maono ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akitaka maporomoko hayo yatumike kufua umeme jambo maono ambayo Rais Dkt. John Magufuli anayatekeleza kwa kuweka jiwe la msingi na haya ni maneno yake.
Katika hatua nyingine Rais Dkt. Magufuli amemwagiza Waziri wa Mali Asili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala kugawa pori la Selou kuwa mbuga ya Taifa ili kudhibiti shuhuli za uwindaji wa wanyama unaofanyika katika pori hilo.
Shirika la Umeme nchini Tanesco linazalisha megawati 1601 ambapo kukamilika kwa mradi wa kufua umeme wa maji rufiji itawezesha Tanzania kuwa na Megawat 3716 huku mahitaji ya ndani ya kiwa ni chini ya megawat 2000.