Rais wa John Magufuli amewasili jijini Pretoria nchini Afrika Kusini ambapo hapo kesho atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa.
Rais Magufuli ambaye ameongozana na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt Jakaya Kikwete na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Philip Mangula, aliwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg na kisha kuelekea Pretoria.
Rais Mteule Cyril Ramaphosa ataapishwa kuwa Rais wa Tano wa Afrika Kusini, katika sherehe zitakazofanyika kwenye uwanja wa Loftus Versfeld jijini Pretoria.
