Rais Magufuli awaapisha Dkt Mahera na Kanali Ibuge

0
185

Rais John Magufuli amewaapisha Dkt Wilson Mahera kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Kanali Wilbert Ibuge kuwa Balozi.

Akizungumza baada ya kuwaapisha Viongozi hao Ikulu jijini Dar es salaam, Rais Maufuli amewataka wafanye kazi kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu na kwa maslahi ya Taifa.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Dkt Mahera na Kanali Ibuge kufanyakazi kwa bidii.