Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mzee Benjamin Mkapa amemtunuku Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa Rais John Magufuli.

Hafla ya kumtunuku Rais Magufuli Shahada hiyo imefanyika jijini Dodoma wakati wa Mahafali ya Kumi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mara baada ya kutunukiwa Shahada hiyo, Rais Magufuli amekipongeza Chuo hicho kwa kutambua mchango wake na kuamua kumpatia Shahada hiyo.
