Rais Magufuli atoa siku 5 kwa waziri wa ujenzi na waziri wa fedha kumlipa mkandarasi kwa ajili ya mradi wa kiwanja cha ndege Mtwara

0
513

Rais Dkt. JOHN MAGUFULI ametoa siku TANO kwa Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi ISACK KAMWELWE na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. PHILIP MPANGO kuhakikisha wanawasilisha fedha asilimia KUMI NA TANO kwa Mkandarasi BEIJING ENGINEERING CONSTRUCTION CO .LTD kwa ajili ya mradi wa upanuzi wa kiwanja cha ndege cha MTWARA.

Rais MAGUFULI ametoa agizo hilo mkoani MTWARA wakati akiweka jiwe la msingi la mradi huo baada ya kupewa taarifa kwamba mkandarasi anadai kiasi cha fedha na kusema sababu za serikali kukarabati uwanja huo ni kuwepo kwa fursa nyingi mkoani humo.