Rais wa John Magufuli amemteua Dkt. Mwinyi Haji kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Haji alikuwa Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar na anachukua nafasi ya Balozi Ramadhani Mwinyi.
Uteuzi wa Dkt. Haji unaanza leo Julai 18, 2020 na anatakiwa kuwepo Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma Julai 20, 2020 saa 4:00 asubuhi.