Rais Magufuli atatua mgogoro wa ardhi Mbozi

0
274

Rais John Magufuli ameagiza Wakazi wa kijiji cha Nanyala wilayani Mbozi mkoani Songwe, kuendelea kulitumia eneo lenye ukubwa wa Ekari 2,115 linalogombewa na Wakazi hao na kiwanda cha Saruji Mbeya.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo aliposimama katika kijiji hicho cha Nanyala na kuelezwa kero hiyo na Mwenyekiti wa kijiji hicho, Philemon Namwema.

Katika maelezo yake kwa Rais Magufuli, – Namwema amesema kuwa, mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu na wamezuiwa kufanya shughuli yoyote, huku Wananchi wengine 23 wakikabiliwa na kesi Mahakamani.

Akitoa uamuzi huo, Rais Magufuli amewaagiza Mawaziri husika kukaa pamoja na kufuta kesi iliyopo Mahakamani na baada ya hapo wamjulishe ili aweze kubadili matumizi ya ardhi katika eneo hilo.