Rais Magufuli arejesha ardhi ya wananchi iliyochukulia na TANROADS

0
600

Rais John Magufuli ameagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkao wa Mbeya kurejesha eneo la Kijiji cha Isyonje, Wilaya Rungwe, mkoani Mbeya kwa Kaya 109 zilizozuiliwa kuendeleza maeneo hayo.

Rais Magufuli amechukua hatua hiyo baada ya kusikia malalamiko ya wananchi kupitia kipindi cha TBC1, Jambo Tanzania, leo asubuhi.

Akizungumza kwa njia ya simu Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila kusimamia zoezi hilo na kuwaacha wananchi waendeleze maeneo yao.

Aidha, ameiagiza TANROADS kukipa kijiji hicho milioni 20 ili kiweze kumalizia ujenzi wa shule ya msingi inayojengwa.

Kwa upande wa wananchi wa kata hiyo wamemshukuru Rais Magufuli kwa huruma yake na kusema kwa miaka mitatu wamesimamisha ujenzi na maendeleo yote katokana na mvutano wa eneo hilo.