Rais Magufuli aongeza siku 20 za kusajili line kwa alama za Vidole

0
313

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya usajili wa laini yake ya simu kwa kutumia alama za vidole na kuwasisitiza Watanzania wote wahakikishe laini zao za simu zinasajili kwa alama za vidole kama ilivyoelekezwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Rais Magufuli amefanya usajili huo Chato Mjini katika Mkoa wa Geita.

Hata hivyo, Rais Magufuli ameongeza siku 20 kuanzia tarehe 01 Januari, 2020 hadi tarehe 20 Januari, 2020 kwa wote ambao watashindwa kusajili laini zao katika kipindi cha kuishia tarehe 31 Desemba, 2019
kama ilivyotangazwa na TCRA kutokana sababu mbalimbali zikiwemo kuugua na kukamilisha upataji wa namba na vitambulisho vya Taifa.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa baada ya muda huo hakuna
kisingizio chochote kitakachokubalika na ameagiza TCRA kuhakikisha laini ambazo hazijasajiliwa zinazimwa.

Amefafanua kuwa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ni muhimu kwa usalama wa nchi ikiwemo kuepusha vitendo vya utapeli na ujambazi vinavyofanywa na wahalifu nchini