Rais Magufuli aomboleza kifo cha Mugabe

0
179

Rais John Magufuli amesema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Rais wa zamani wa Zimbabwe, -Robert Mugabe.

Katika mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Magufuli amesema kuwa Afrika imepoteza mmoja wa viongozi Jasiri, Shupavu, Mwanamajumui wa Afrika na aliyekataa ukoloni kwa vitendo.

Mugabe amefariki Dunia nchini Singapore alikokua akipatiwa matibabu na amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 95.

Ameiongoza Zimbabwe kuanzia mwaka 1980 mpaka mwaka 2017.