



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa,mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.Rais Ramaphosa amewasili hapa nchini jana jioni kwa Ziara ya Kitaifa ya siku 3 na baada ya hapo atahudhuria Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika viunga vya Ikulu,leo jijini Dar .
