Rais Magufuli amnasua Mchungaji Msigwa gerezani

0
408

Rais John Magufuli amemlipia Shilingi milioni 38 Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, kati ya shilingi milioni arobaini alizotakiwa kulipa faini baada ya kuhukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawailiano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, ndiye aliyefika katika mahakama hiyo akiwa amefuatana na mjomba wa Mchungaji Msigwa kwa ajili kukamilisha taratibu za kulipa faini hiyo.

Hivi karibuni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwahukumu kulipa faini ya jumla ya shilingi milioni 350 au kifungo cha miezi mitano kwa kila kosa viongozi waandamizi wa CHADEMA pamoja na aliyekua Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt Vicent Mashinji baada ya kuwakuta na hatia katika makosa kumi na mawili.

Katika faini hiyo Mchungaji Msigwa alitakiwa kulipa shilingi milioni arobaini.