Rais Magufuli amjulia hali Zitto Kabwe baada ya ajali

0
381

Rais Dkt. Magufuli amempigia simu na kumpa pole Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe aliyepata ajali ya gari jana mkoani Kigoma.

Dkt. Magufuli amemuombea heri ili apone haraka na pia amewashukuru madaktari na wauguzi wa Kituo cha Afya cha Kalya na Hospitali ya Maweni kwa matibabu waliyompa.

Zitto Kabwe alipata ajali ya gari jana akiwa njiani akitokea Kata ya Kalya kuelekea Lukoma kwenye kampeni katika Jimbo la Kigoma Kusini leo Jumanne Oktoba 6, 2020.