Rais John Magufuli amekwenda nyumbani kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo Msasani jijini Dar es salaam kumpa pole, kufuatia kifo cha mtoto wake Nelson.
Nelson Mabeyo aliyekuwa Rubani, amefariki dunia hii leo baada ya ndege ndogo aliyokuwa akiiendesha ya kampuni Auric Air kuanguka muda mfupi baada ya kupaa katika kiwanja kidogo cha ndege cha Seronera wilayani Serengeti mkoani Mara.
Nelson na mwenzake Nelson Orutu ambaye ni Rubani Mwanafunzi, walikua wakielekea katika kiwanja kingine cha ndege cha Grumeti kwa ajili ya kupakia abiria.