Rais Magufuli Afika Kutoa Pole Kwa Mbowe Aliyefiwa Na Kaka Yake

0
277

Rais  John  Magufuli leo asubuhi amefika na kutoa pole kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe,  baada ya  kufiwa na kaka yake, Meja Jenerali Mbowe,  Julai 28, 2019. Msiba upo nyumbani kwa marehemu Salasala jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya Ikulu ya leo Jumanne Julai 30, 2019,  imesema Rais  Magufuli amekutana na kiongozi wa familia hiyo, Freeman Mbowe, ambapo ameshiriki sala ya kumuombea marehemu Meja Jenerali Mbowe.

Baada ya sala hiyo na baadhi ya wanafamilia ya Marehemu Mbowe, Rais Magufuli ameitaka familia hiyo kuendelea kuwa na umoja kama ilivyokuwa wakati wa Uhai wa Marehemu Mbowe na kumtanguliza Mungu mbele.

Akizungumza katika Msiba huo, Mkuu wa Majeshi Jenerali Venancy Mabeyo amesema licha ya Kustaafu lakini bado Marehemu Mbowe alikuwa akiendelea kulishauri Jeshi katika kutekeleza majukumu yake kwa weledi.

Janelari Mabeyo ameseama, katika utumishi wake wa Miaka 36 na siku 27 Jeshini, Marehemu Meja Jenerali Mbowe alikuwa msimamizi mzuri wa fedha za Jeshi hilo.

Marehemu Meja Jenerali Mbowe amezaliwa Mwaka 1953 na kujiunga na Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania mwaka 1973 na amestaafu utumishi Jeshini mwaka 2009.