Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza Soko Kuu la Nachingwea

0
177

Rais John Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika Soko Kuu la wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi na kubaini kuwa ujenzi wa soko hilo hauendani na thamani ya fedha zilizotumika katika ujenzi huo hadi sasa.

Ziara hiyo ya Rais Magufuli imetokana na malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya Wakazi wa wilaya ya Nachingwea ambao walimuomba kukagua ujenzi huo ili ajiridhishe baada ya kutokubaliana na maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea.

Katika ziara hiyo, Rais Magufuli amejionea ujenzi usioridhisha wa Soko hilo Kuu la wilaya ya Nachingwea na kuwashukuru Wakazi wa wilaya hiyo kwa kumueleza ukweli kuhusu ujenzi wa soko lao.

Rais Magufuli ameahidi kusimamia kwa karibu ujenzi wa soko hilo ili likamilike na Wafanyabiashara waendelee kulitumia.