Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti watatu

0
493
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wenyeviti watatu watakaoongoza bodi za taasisi mbili za serikali na moja ya ubia wa serikali na sekta binafsi.

Kwanza, Rais Magufuli amemteua Gabriel Pascal Malata kuwa mwenyekiti na mjumbe wa kuiwakilisha serikali katika bodi ya Kampuni ya Airtel Tanzania Ltd.

Malata ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.

Pili, Rais Magufuli amemteua Prof. Martha Qorro kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (Institute of Rural Development Planning – IRDP).

Prof. Martha Qorro ni Profesa Mshiriki wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Tatu, Rais Magufuli amemteua Prof. Joseph Rwegasira Buchweshaija kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hawa umeanza tarehe 30 Januari, 2020.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
31 Januari, 2020