Rais Magufuli afanya uteuzi wa viongozi wapya

0
462
Dkt. Zainab Abdi Seraphin Chaula ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Mawasiliano.

Rais John Magufuli amemteua Dkt. Zainab Chaula kuwa Katibu Mkuu wa Mawasiliano.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Chaula alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na amechukua nafasi iliyoachwa na Dkt. Maria Sasabo ambaye amestaafu.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Prof. Mabula Mchembe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Kabla ya uteuzi huo, Prof. Mchembe alikuwa Msaidizi wa Rais katika masuala ya afya.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof. Abel Makubi kuwa Mganga Mkuu wa Serikali (Chief Medical Officer).

Kabla ya uteuzi huo, Prof. Makubi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando na amechukua nafasi iliyoachwa na Prof. Mohamed Bakari Kambi ambaye amestaafu.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 22 Aprili, 2020.