Rais Magufuli afanya uteuzi wa viongozi sita wa wilaya

0
424

Rais John Magufuli amefanya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya mmoja na Wakurugenzi wa Halmashauri watano kama ifuatavyo;

Kwanza, Rais Magufuli amemteua Lauteri Kanoni kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe. Kabla ya uteuzi huo, Kanoni alikuwa Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Serikali za Mitaa katika Mkoa wa Songwe na anachukua nafasi ya Ally Kasinge.

Pili, Rais Magufuli amemteua Bashir Mhoja kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mkoani Iringa. Kabla ya uteuzi huo, Mhoja alikuwa Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mkoani Geita na anachukua nafasi ya Robert Masunya.

Tatu, Rais Magufuli amemteua Ramadhan Possi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani. Kabla ya uteuzi huo, Possi alikuwa Afisa Mipango katika Jiji la Tanga Mkoani Tanga na anachukua nafasi ya Amina Kiwanuka ambaye amestaafu.

Nne, Rais Magufuli amemteua Baraka Zikatimu kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora. Kabla ya uteuzi huo, Zikatimu alikuwa Afisa Mipango katika Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli Mkoani Tanga na anachukua nafasi ya Margareth Jonathan Nakainga ambaye amestaafu.

Tano, Rais Magufuli amemteua John Nchimbi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara. Kabla ya uteuzi huo, Nchimbi alikuwa Afisa Rasilimali Watu katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Mkoani Morogoro.

Sita, Rais Magufuli amemteua Emmanuel Johnson kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga. Kabla ya uteuzi huo, Johnson alikuwa Afisa Elimu wa Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza.

Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe 07 Julai, 2020.