Rais John Magufuli amemteua Onorius Njole kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria.
Uteuzi wa Njole umeanza leo Mei 23.
Kabla ya uteuzi huo, Njole alikuwa Mkurugenzi wa Sheria na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).
Njole anachukua nafasi ya Sara Barahomoka ambaye anastaafu.
