RAIS MAGUFULI ABARIKI UWANJA WA TAIFA KUITWA “MKAPA STADIUM”
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameridhia uwanja wa Taifa kuitwa ‘Mkapa Stadium’ kama sehemu ya kuenzi mambo aliyoyafanya rais wa awamu ya tatu Hayati Benjamin William Mkapa.
Rais Magufuli amesema amepokea jumbe nyingi kutoka sehemu mbalimbali zikimuomba akubali kuuita uwanja wa taifa ‘Mkapa Stadium’.
“Mzee Mkapa aliujenga uwanja mkubwa wa michezo, kwa sasa wengi wanataka uwanja ‘Mkapa Stadium’, mzee Mkapa alikuwa hapendi vitu viitwe kwa jina lake, lakini kwa kuwa hawezi kuniadhibu chochote amelala hapo na kwa kuwa nimepata meseji nyingi nimekubali natamka rasmi uwanja ule uitwe ’Mkapa Stadium’