Rais Magufuli abadili uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe

0
594

Rais John Magufuli amefanya mabadiliko ya uteuzi alioufanya Julai 17, 2020 ambapo amemteua Mhandisi Marwa Rubirya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Rubirya alikuwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) katika Mkoa wa Mwanza.

Mhandisi Rubirya ameteuliwa baada ya Jumanne Fhika ambaye atabaki Ofisi ya Rais kuendelea na majukumu yake.

Uteuzi wa Rubirya umeanza leo Julai 19, 2020 na anatakiwa kuwepo Ikuku ya Chamwino, Dodoma kesho saa nne asubuhi.