Rais kuunda wizara inayoshughulikia Jinsia, Maendeleo na Wanawake

0
157

Rais Samia Suluhu Hassan amesema ana mpango wa kuitenga wizara itakayoshughulikia Jinsia, Maendeleo, Wanawake na wizara ya afya, lengo likiwa ni kuimarisha utekelezaji wa mipango na sera.

Rais Samia Suluhu Hassan ameelezea mpango huo mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa kamati ya ushauri ya kitaifa kuhusu utekelezaji wa ahadi za nchi kwenye Jukwaa la Kizazi chenye Usawa.

Amesema amefikia uamuzi huo baada ya kuona jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali pamoja na mipango na sera zote zilizowekwa kwa ajili ya kuleta mabadiliko katika eneo la Jinsia na Wanawake kutofikia mahali ambapo Serikali itanataka.

Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza kuwa atamshawishi pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi ili naye afanye kama alivyoamua yeye..