Rais Kulihutubia Bunge Nov 13

0
291

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli atalihutubia Bunge Ijumaa Novemba 13,2020 kuashiria kuanza rasmi kwa shughuli za utendaji wa viongozi waliochaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi mkuu 2020.
Taarifa hiyo imetolewa Bungeni jijini Dodoma na Spika Job Ndugai, alipokuwa akihitimisha kikao cha pili cha mkutano wa kwanza wa Bunge la 12.
Awali wabunge waliendelea kuapa kiapo cha uaminifu Bungeni.