Rais: Kitabu Kitafsiriwe kwa Lugha ya Kiswahi

0
183

Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza Chama Cha Wanasheria Na Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) na Wadau wa sheria kutafsiri kitabu cha ‘TANZANIA GENDER BENCH BOOK ON WOMEN’S RIGHTS’ kwenda lugha ya Kiswahili

“Naomba nitoe rai kwa TAWJA na wadau wote walioshiriki katika uandaaji wa kitabu hiki kuhakikisha kuwa kinatafsiriwa kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili ili watu wengi zaidi wakisome lakini pia kukamilika kuandikwa kwa kitabu hichi isiwe mwisho kiwe kinapitiwa muda baada ya muda na kuongeza yale ambayo yanajitokeza jinsi tunavyo kwenda” Rais Samia Suluhu Hassan

Rais Samia ametoa agizo hilo wakati akizindua kitabu kinachoitwa ‘TANZANIA GENDER BENCH BOOK ON WOMEN’S RIGHTS’ kilichoandaliwa na Chama Cha Wanasheria Na Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) ikiwa ni Mwongozo kwa majaji na mahakimu kuhusu haki za wanawake na watoto nchini

Rais Samia Samia Suluhu Hassan amesisitiza ili serikali iweze kutimiza kikamilifu malengo yaliowekwa kama nchi katika kuwahudumia Watanzania na kuwaletea maendeleo inabidi kutumia lugha inayoeleweka na wengi hususan kwenye mifumo ya utoaji wa haki unaosisitiza usawa kwa watu wote bila kujali hali zao za kijamii na kiuchumi

“Naomba niwasisitize kutumia lugha yetu ya Kiswahili katika kuandika mienendo ya masharti na hukumu kwani tayari Bunge limeshafanya marekebisho ya sheria kuruhusu matumizi ya kiswahili katika sheria zetu
“Najua ni kazi nzito msamiati [ma-terminology] yenu kuyatafsiri Kiswahili lakini anzeni hata kama utaandika kwa kiswahili katikati ukaweka kingereza kwa msamiati [terminology] ya kimahakama lakini mtu atauliza hili neno maana yake nini ataambiwa mnapokosa tafsiri wekeni maneno yakingereza maana hata Kiswahili kina maneno yakutohoa” Rais Samia Samia Suluhu Hassan