Rais John Magufuli akemea makandarasi wazembe

0
574

Rais JOHN MAGUFULI ameitaka Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano kutowapa kazi wakandarasi wasiotekeleza majukumu yao kikamilifu.

Rais MAGUFULI ametoa agizo hilo Mkoani MTWARA wakati wa uzinduzi wa barabara ya kiuchumi ya MTWARA-MLIVYATA-TANDAHIMBA-NEWALA hadi MASASI ambapo pia ameitaka Bodi ya Wakandarasi nchini kuwafukuza kazi wakandarasi wasiofanya kazi vizuri.