Rais Dkt. Mwinyi ziarani Falme za Kiarabu

0
163

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameondoka nchini leo kuelekea Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) kwa ziara ya siku tatu.
 
Ziara hiyo ya Rais Dk. Mwinyi ni kufuatia mwaliko maalumu wa Kiserikali aliopewa na Mrithi wa Mtawala wa Abudhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi wa Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E), Sheikh Mohammed  bin Zayed Al Nahyan.
 
Dk. Mwinyi anatarajia kuanzia ziara yake hiyo nchini Abudhabi ambako atahudhuria maadhimisho ya wiki maalum ya kushajihisha maendeleo endelevu inayoadhimishwa kila mwaka nchini humo.

Pia, atahudhuria mkutano wa wakuu wa Nchi na Serikali mbalimbali duniani utakaofanyika Dubai.
 
Katika ziara hiyo, Rais Dk. Mwinyi amefuatana na viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.